Rais wa pekee mwanamke barani Afrika, kutoka nchini Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim amekataa kujiuzulu licha ya kuandamwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha.

Gurib-Fakim amekanusha madai kuwa alitumia mamilioni ya dola kwa matumizi binafsi kwa kutumia kadi ya benki ya shirika la msaada.

Aidha, Ofisi yake imesema kuwa matumizi hayo yalikuwa ni bahati mbaya na fedha zote zilizotumika zimerudishwa katika Akaunti ya Serikali.

“Mheshimiwa Ameenah Gurib-Fakim, hana hatia yoyote na ametoa ushahidi wakutosha hivyo amekataa wazo lolote la kuachia madaraka.” taarifa kutoka ofisi ya rais imesema.

Hata hivyo, Ofisi yake imesema kuwa dola za Kimarekani 27,000 zimerudishwa na rais Gurib-Fakim, hivyo suala hilo liendeshwe kisheria.

 

Watu 40 wauawa, nyumba 1000 za chomwa moto
Mwanasayansi maarufu afariki dunia

Comments

comments