Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ameomnyesha kuguswa na kifo cha aliyewahi kuwa mlinda mlango wa timu ya taifa hilo (The Cranes) Abel Dhaira, ambaye alifariki dunia siku mbili zilizopita huko nchini, Iceland alikokuwa anasumbuliwa na kansa ya utumbo.

Rais wa Uganda, ameopnyesha kuguswa huko, baada ya kuandika ujumbe wa majonzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, halia mbayo imeonyesha amesikia na kuwa sehemu ya walioumizwa na kifo cha mlinda mlango huyo  ambaye aliwahi kuidakiwa klabu ya Simba ya Tanzania, URA, Express na timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.

Katika ujumbe huo, Museveni amesema serikali yake itagharimia kila kitu ikiwemo kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka nchini Iceland hadi nchini Uganda, pamoja na mazishi, huku akiwapa pole wanafamilia wa Dhaira na familia yote ya wapenda michezo katika kipindi hiki cha kigumu.

Jurgen Klinsmann Kuuza Jumba Lake La Kifahari
Utafiti: Karibu Nusu ya wanawake wanaojiuza wana Virusi vya Ukimwi