Rais wa Zambia, Edgar Lungu, ametangaza kufungua rasmi mpaka na Tanzania na kuruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Rais Lungu ametoa agizo hilo jana jioni wakati akilihutubia taifa na kuagiza wananchi waendelee na shughuli zao huku wakifuata maoni na ushauri wa Wataalam katika kujikinga na virusi vya Corona.

Ikumbukwe kuwa Zambia ilifunga mpaka wake na Tanzania tangu Mei 11 huku wilaya ya Nakonde ikipigwa ‘lockdown’ ikiwa ni hatua ya kutathmini njia za kuzuia maambukizi yaliyokuwa yakiongezeka kwa kasi ndani ya Nakonde.

Ndege yaanguka kwenye makazi ya watu Pakistan
Sikukuu ya Eid: Benki ya Exim yatoa msaada kwa watoto yatima mikoa minne