Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Rally Bwalya amesema kucheza soka nchini Afrika Kusini, ilikua ni sehemu ya ndoto zake tangu akiwa na umdi mdogo.

Bwalya aliyeagwa rasmi Simba SC siku kadhaa zilizopita, amesema malengo yake makubwa yalikua ni kucheza Ligi Kuu ya Afrika Kusini ‘PSL’, hivyo hana budi kumshukuru mungu kwa kukamilisha ndoto zake baada ya kusajiliwa na Amazulu FC.

Amesema anatambua ana kazi kubwa ya kufanya kwa kushirikiana na wenzake klabuni hapo, baada ya kufanya mambo makubwa akiwa na Simba SC ya Tanzania kwa misimu miwili.

“Kujiunga na Amazulu kwangu ni mafanikio makubwa kwani nimekuwa nikiitazama na kuifuatilia kwa muda mrefu Amazulu FC, inajulikana sana kwetu Zambia kwa sababu watu wengi wanatazama PSL.

“Ni timu ambayo siyo mpya kwangu, jambo kubwa ni kuisaidia klabu yangu kwa jitihada zote kwani kila mchezaji anakuwa na malengo yake na kuisaidia klabu kufikia malengo yaliyowekwa kwa msimu husika,” amesema Bwalya

Akiwa Simba SC, Bwalya alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa Ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2020/21, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, Ngao ya Jamii pamoja na Kufika hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa na Kombe la na Shirikisho Barani Afrika.

Rais Samia amtaja Mama Mkapa kwenye safari yake ya siasa
Ahmed Ally awaomba radhi mashabiki Simba SC