Hatimaye Kiungo kutoka nchini Zambia Clatous Chama ametambulishwa rasmi na Mabingwa Soka Tanzania Bara Simba SC katika usajili wa Dirisha Dogo ambao utafikia kikomo kesho Jumamosi (Januari 15).

Chama ametambulishwa Simba SC kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo leo Ijumaa (Januari 14) Mchana, huku akikaribishwa kwa maneno ‘Clatous Chama Welcome Home (Karibu nyumbani, Clatous Chama)’.

Hatua hiyo inasitisha uvumi wa Tetesi za usajili wa kiungo huyo klabuni hapo, baada ya kuripotiwa hakuwa na wakati mzuri nchini Morocco, baada ya kusajiliwa na RS Berkane, hivyo alitamani kurudi Tanzania.

Kwa kipindi cha miezi mitatu Tetesi za Chama kurejea Simba SC zilishika hatamu, huku Young Africans wakitajwa walikua kwenye mpango wa kuingilia dili lake la kurejea Msimbazi. Simba SC ilimuuza Chama mwanzoni mwa msimu huu, sambamba na kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Msumbiji Jose Luis Miquissone aliyetimkia kwa Mabingwa wa Soka Afrika Al Ahly ya Misri.

Young Africans kuijibu Simba SC, kutangaza kifaa cha kimataifa
Haji Manara: Coastal Union inategemea siasa za mpira