Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA), Suleiman Haji “Kibabu”, amemtangaza Ravia Idarous Faina kuwa mshindi wa urais wa ZFA kwenye uchaguzi uliofanyika leo hii April 14 Gombani kisiwani Pemba.

Akitangaza matokeo hayo kwenye ukumbi wa Gombani kisiwani Pemba Kibabu  mshindi wa Urais wa Chama Cha Soka Zanzibar  (ZFA) Taifa kuwa Ravia Idarous Faina ambapo ametetea nafasi yake ya urais kwa kupata asilimia 88.68 katika uchaguzi wa chama hicho uliofanyika leo hii.

Ravia ameweza kutoka kidedea kwa kupata kura 47 kati ya kura 53 zilizopigwa katika uchaguzi huo na kumpita mpinzani wake Salum Baus ambae alipata kura sita (6) tu pekee.

Kwa upande wa nafasi ya Makamo wa Rais Pemba, nafasi hiyo imerudi tena kwa Ali Mohammed Ali alieshindana na Suweid Hamad Makame kwa kupata kura 46 sawa na asilimia 86.79 ambapo mpinzani wake amepata kura saba (7) sawa na asilimia 13.21.

Nafasi ya Makamo wa Rais Unguja imeenda kwa Mzee Zam Ali ambae amepata kura 37 sawa na asilimia 69.81 .

Katika uchaguzi huo nafasi ya Makamo wa Rais Unguja iligombewa na wagombea watatu ambapo Mohammed Masoud alipata kura 11 sawa na asilimia 20.76 na Ali Nassor Salum Mkweche alipata kura tano ikiwa ni sawa na asilimia 9.43.

Viongozi ambao wamechaguliwa wanatarajia kutumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu kufuatia mwaka 1 na nusu uliopita soka hilo kuwepo Mahakamani .

Kobe Bryant "The Black Mamba" Astaafu Kwa Heshima
Kocha Wa Amavubi Awataka Azam FC Kukaza Wakifika Tunisia