Watumishi wa umma wametakiwa kutokulalamika badala yake waongeze juhudi za utendaji kazi ili kuweza kuboresha huduma wanazozitoa kwa jamii ziweze kuonekana kwa macho na kwa maneno.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi katika baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya Itigi ambapo amesema kuwa watunishi na watendaji wanatakiwa kupunguza muda wa kukaa vikao ili waende kuwatumikia wananchi.

Amesema kumekuwa na tabia ya kulalamika ambayo pia inaambukiza kwa watumishi na watendaji wengine badala ya kutoa suluhisho kwa changamoto ambazo zitawasaidia wananchi kutatua kero mbalimbali.

Aidha, Dkt Nchimbi ameongeza kuwa watendaji na madiwani wasitumie muda mwingi ofisini pamoja na kusubiria taarifa za makaratsi ambazo hazina uhalisia wa matukio na hali halisi inayoendelea kwa wananchi.

Vile vile, amesema watumishi, watendaji na madiwani wanapaswa kuzingatia kuwaheshimu, kuwatambua, kuwathamini na kutowadanganya wananchi katika kuwatumikia kwakuwa wananchi wana uelewa wa kutosha juu ya mambo mbalimbali.

Hata hivyo, ameongeza kuwa madiwani wasimamie kwa umakini miradi na shughuli za serikali ili thamani ya fedha iweze kuonekana kwa miradi hiyo huku akiwashauri kumtumia mkaguzi wa ndani kama kioo cha kuangalia dosari zao na kuzirekebisha mapema.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Nje wa Hesabu za Serikali  Anna Kakunguru ameishukuru halmashauri ya Itigi  kwa ushirikiano na kuwaasa wasiwe wataalamu wa kujibu hoja bali wawe wataalamu wa kuzuia hoja.

 

Craig Shakespeare Awakaribisha AS Roma
RC Rukwa atoa tahadhari kwa wasimamizi wa fedha za ukarabati shule Kongwe