Wavuvi na Wachimba Madini wadogo wadogo wamepewa muda wa siku nane kuchukua vitambulisho vitakavyo wawezesha kutambulika rasmi kama wajasiliamali wadogo wadogo ili waweze kufanya shughuli halali za uzalishaji mali bila kusumbuliwa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela wakati wa ziara aliyoifanya Wilayani Songwe ambapo ametembelea kambi ya wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Saza na wajasiliamali wa Uvuvi katika kambi ya Sabasaba pembezoni mwa mto Rukwa.

Amezitaka halmashauri za Mkoa wa Songwe kuhakikisha zinasimamia vizuri ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo wadogo ili kuepuka udanganyifu na kuhakikisha kila Mjasilimali anatambulika kwa kupata kitamblisho hicho.

“Mjasiliamali mdogomdogo unayefanya shughuli yeyote halali inayokuingizia kipato na hulipi kodi TRA serikali inataka kukutambua hivyo basi unatakiwa kuchukua kitambulisho ili usisumbuliwe,”amesema Brig. Jen. (Mst) Mwangela

Kwa upande wake Afisa wa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Omary Iddi amesema kuwa wajasiliamali wadogo wadogo ambao kipato chao kwa siku wanapata chini ya shilingi milioni nne kwa mwaka wanapaswa kuchukua kitambulisho cha Ujasiliamali ili nao waweze kuchangia pato la taifa.

Wajasiliamali wadogo wanaoishi kwenye kambi ya Uvuvi ya Sabasaba, Wachimbaji wadogo wa madini wa Saza na wajasiliamali wegine Wilayani Songwe wamezipongeza juhudi za serikali za kuweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi kwa manufaa ya maendeleo ya Taifa.

 

Zaidi ya Sh. Bil. 500 zimelipwa kwa wakulima wa Korosho- Majaliwa
Wajasiliamali Dodoma waipa siku 14 Halmashauri kuzuia magari ya mizigo

Comments

comments