Uongozi wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, umedhamiria kumsainisha mkataba mpya meneja wao kutoka nchini Ufaransa Zinedine Zidane.

Mtandao wa AS.com, umeripoti kuwa Zizou atasainishwa mkataba mpya ambao utamuwezesha kupokea mshahara mara mbili ya anaoupokea hivi sasa.

Mkataba wa awali ambao Zizou aliusaini mara baada ya kukabidhiwa jukumu la kuwa mkuu wa benchi la ufundi la Real Madrid mwishoni mwa mwaka 2015, unamuwezesha kulipwa mshahara wa Euro milion 2.7 kwa mwaka, hivyo mpango uliopo utamsogeza hadi katika kiasi cha Euro milioni 5.5 kwa mwaka.

Lengo kubwa la uongozi wa Real Madrid kufanya hivyo, ni kutaka kutengeneza mazingira ya kuendelea kuwa na Zidane ambaye anatarajiwa kuwa meneja borazaidi barani Ulaya katika siku za usoni.

Everton Wabadili Gia Angani, Wapanga Kumbakisha Lukalu
Luis Suarez: Daima Nitaipenda Na Kuithamini Liverpool