Kufuatia kifo cha Baba mzazi wa mke wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mzee Rashid Mkwachu aliyefariki dunia jana Alhamisi, Julai 19, 2018 majira ya saa tatu asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam, mjukuu wa marehemu, Ridhiwani Kikwete ametaja ugonjwa uliomuua babu yake kuwa ni moyo na hali ya uzee.

“Babu yetu alikuwa mzee sana, zamani utunzaji wa kumbukumbuku haukuwa mzuri, lakini anakadiria kuwa ameishi kwa miaka 104 au 107. Sisi hatuna kubwa la kusema lakini tunadhani tu kwamba umri wake ulikuwa umefika. Kuna wakati alikuwa anasumbuliwa na moyo kushindwa kusukuma damu vizuri, presha ya kupanda na ya kushuka.”

“Nitamkumbuka babu kwa kuwa alipenda sana kutupigisha stori hasa za mpira, simulizi na maisha yake ya kila siku, ni vitu vingi alikuwa akinishauri enzi za uhai wake, mengi yalikuwa ni kunitakia kheri kwa yale niliyokuwa nikiyafanya,” amesema Ridhiwani.

Kwa mujibu wa taarifa Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni msemaji wa familia, msiba huo upo nyumbani kwa Dkt. Jakaya Kikwete maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam na mazishi yatafanyika leo Ijumaa, Julai 20, 2018 katika Makaburi ya Kisutu majira ya saa 10:00 jioni.

Saba kupigwa panga Arsenal, kuongezwa wengine wawili
Miss Ilala wampongeza DC Mjema

Comments

comments