Hatimaye Serikali ya Uingereza imebaini chanzo kilichopelekea jengo refu (ghorofa) kuteketea kwa moto jijini London.

Ripoti ya uchunguzi wa tukio hilo imeeleza kuwa chanzo ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye jokofu katika chumba kimoja cha jengo hilo. Imeeleza kuwa chanzo hicho hakikufanywa kwa makusudi na mtu yeyote.

Watu sabini na tisa wanahofiwa kupoteza maisha katika jengo hilo lililoteketea kwa moto likiwa na nyumba 151.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa tayari limeshafanya mawasiliano na kampuni iliyotengeneza jokofu hilo, pamoja na kitengo cha biashara, nishati na sera za viwanda kuhusu chazo hicho.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa aina hiyo ya jokofu haijawahi kulalamikiwa na mteja yeyote.

Mataifa ya Kiarabu yaitaka Qatar kukifunga kituo cha habari cha Aljazeera
Chai ya rangi yaua mume, mke