Aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Roberto Soldado, ni miongoni mwa wachezaji watano wa klabu ya Galatasaray waliofungiwa, kufuatia ugomvi uliozuka wakati wa mchezo wa ligi ya Uturuki dhidi ya Fenerbahce uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wengi zaidi nchini Uturuki, ulimalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Soldado mwenye umri wa miaka 33, ambaye alijiunga na Fenerbahce akitokea nchini Hispania kwenye klabu ya Villarreal mwaka 2017, alikua sehemu ya wachezaji watatu walioadhibiwa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada zogo kutokea.

Mamlaka ya soka nchini Uturuki imetangaa adhabu ya kumfungia Soldado michezo sita, baada ya kufuatilia kwa ukaribu ripoti ya mwamuzi na kurudia tukio la ugomvi kwa njia ya televisheni.

Mchezaji Jailson Siqueira wa Fenerbahce, ameadhibiwa kwa kufungiwa michezo minane huku Badou Ndiaye wa Galatasaray akifungiwa michezo mitano.

Meneja wa Galatasaray Faith Terim amefungiwa michezo saba, baada ya kuthibitika alimtolea maneno machafu mwamuzi na baada ya mchezo huo aliendelea kutoa maneno ya kejeli alipozungumza na waandishi wa habari.

Meneja msaidizi Hasan Sas, naye ameadhibiwa michezo minane, kutokana na kitendo chake cha kuwashambulia viongozi wa benchi la timu pinzani.

Viungo wa Galatasaray Garry Mendes Rodrigues na Ryan Donk wamefungiwa michezo mitatu kila mmoja.

Wakati huo huo timu zote zimetozwa faini, kutokana na kushindwa kuzuia hasira za wachezaji, hadi kupelekea zogo ambalo lilitokea mara baada ya mchezo kumalizika, na chanzo chake kinatajwa kuwa upinznai uliopitiliza baina ya manguli hao wa soka nchini Uturuki.

Video: Magufuli amfukuza kazi Kidata, Amvua ubalozi, Zitto aibua madudu mengine bungeni
Danny Welbeck azua hofu Emirates Stadium

Comments

comments