Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki, Luis Nani, huenda akarejea kucheza soka katika ligi ya England, kufuatia mipango inayoandaliwa na meneja mpya wa klabu ya Everton, Ronald Koeman.

Nani, alijiunga na klabu ya Fenerbahce, msimu uliopita akitokea Man Utd baada ya kuonekana hakidhi mahitaji ya aliyekua meneja wa klabnu hiyo Louis Van Gaal ambaye pia aliwahi kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu ya Sporting Lisbon ya nchini kwao Ureno.

Koeman, anaamini  Luis Nani atafanikisha azma ya kusaidia baadhi ya mipango yake endapo atamsajili huko Goodison Park, ambapo kumewekwa mikakati madhubuti ya kufanya vyema kwa msimu wa 2016-17 ambao umepangwa kuanza mwezi August mwaka huu.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29, anaweza kuondoka katika klabu ya Fenerbahce kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 6.5, kutokana na mkataka wake unavyoeleza.

Hata hivyo Koeman, huenda akapata upinzani katika hatua ya usajili wa Nani, kufuatia klabu ya Valencia ya nchini Hispania kuonyesha dhamira ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo, ambaye kwa sasa yupo nchini Ufaransa akiitumikia timu yake ya taifa ya Ureno katika fainali za Euro 2016.

Wakimbizi 200 wa Boko Haram Wafa kwa Njaa
Mzamilu Yasin Amtumia Salam Jonas Mkude