Mchezaji anayetamba kwasasa, Cristiano Ronaldo ameendelea kufanya kile anachopenda cha kuwanyamazisha mashabiki na wapenzi wa Juventus kwa kuzifumania nyavu.

Jana usiku alifunga magoli mawili kati ya matatu ambayo Real Madrid waliwatundika Juventus katika michuano ya kombe la mabingwa wa Ulaya.

Mashabiki wa Juventus wakijua kuwa mbaya wao ni Ronaldo walianza kwa kumzomea lakini kelele zao zilipungua dakika ya 3 alipofunga goli la kwanza.

Goli la pili, alilofunga kwa ‘tik-tak’, liliwafanya watazamaji wote, wakiwemo wa Juventus, kumshangilia Cristiano Ronaldo. Mpira ulipokwisha Buffon alimkumbatia Ronaldo na kumpongeza.

 

Waliomteka Padri wadai pesa kumuachia
Serikali yaomba kesi ya Mbowe na wenzake iende haraka

Comments

comments