Wachezaji Marcus Rashford, Andros Townsend pamoja na Jack Wilshere wamekua miongoni mwa waliotajwa na kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hogdson mapema hii leo kwa ajili ya kuunda kikosi cha The Three Lion, kitakachoshiriki fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016).

Hodgson ametaja kikosi chake, ikiwa ni siku moja baada ya msimu wa 2015-16 kufikia kikomo huko nchini England, lakini amewashangaza wengi kwa hatua ya kumuacha mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott.

Kiungo na nahodha wa majogoo wa jiji Liverpool, Jordan Henderson naye ni miongoni mwa waliotajwa na kocha huyo ambaye amebeba dhamana ya kuitafutia heshima England katika fainali hizo, ambazo zitaanza kuunguruma mwezi Ujao nchini Ufaransa.

Hata hivyo Jordan Henderson pamoja na Wilshere, imewachukua muda mfupi kuonekana uwanjani wakiwa na vikosi vya klabu zao za Arsenal na Liverpool, baada ya kupona majeraha yaliyokua yanawakabili, tofauti na ilivyo kwa Walcott.

Mwingine aliyewashangaza wengi kwa kuitwa katika kikosi cha The Three Lion, ni kiungo mshambuliaji wa klabu ya Newcastle Utd iliyoshuka daraja Townsend sambamba na mshambuliaji kinda wa Man Utd, Marcus Rashford.

England itaingia kambini kujiandaa na fainali za Euro 2016, sanjari na kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Uturuki pamoja na Australia, Mei 22 na 27.

Kikosi kamili kilichotajwa na kocha Hodgson upande wa makipa yupo, Joe Hart, Fraser Forster, Tom Heaton.

Mabeki: Kyle Walker, Nathaniel Clyne, John Stones, Gary Cahill, Chris Smalling, Ryan Bertrand na Danny Rose.

Viungo: Eric Dier, Jack Wilshere, Fabian Delph, James Milner, Adam Lallana, Jordan Henderson, Dele Alli, Raheem Sterling, Ross Barkley, Andros Townsend na Danny Drinkwater

Washambuliaji: Wayne Rooney (c), Daniel Sturridge, Harry Kane, Jamie Vardy na Marcus Rashford

N'Golo Kante Ajipeleka Kwa Babu Arsene Wenger
Rais Wa Inter Milan Ampigia Magoti Roberto Mancini