Tunapolala, ubongo wetu unapata wakati wa kutunza kumbukumbu na kufanyia kazi taarifa ilizonazo pia ni muda ambao sumu au uchovu uondoka katika miili yetu na kuruhusu kufanya kazi vizuri tunapoamka.

Hivyo inashauriwa kulala kwenye chumba chenye giza nene kwani uwepo wa mwanga kwenye chumba cha kulala kinaingilia uzalishaji wa kichocheo cha melatonini ambacho huusika katika kukufanya usinzie. Kupungua kwa uzalishaji wa homoni ya melatonin huweza kuleta athari kubwa kwa afya ya mtu.

Kama ambavyo utafiti unavyosema kuna uhusiano mkubwa kati ya upungufu wa melatonin na kuongezeka kwa hatari ya kuugua saratani ya matiti, miaka ya nyuma kabla teknolojia haijakua mababu zetu walilala masaa 12 wakiwa gizani kabisa, leo hiii kutokana na uvumbuzi wa umeme na taa, tumejikuta masaa 16 tukiyatumia kwenye mwanga na masaa 6 tu tukitumia kwenye giza na tena pakiwa mwanga hafifu kwa nje ukiendelea kuwaka.

Aidha, Dr Naiman ambaye ni mwanasaikologia kutoka Marekani anasema “usingizi siyo tu kitendo cha kutokuamka, hii ni tafsiri isiyo sahihi miongoni mwa watu kwenye dunia yetu kwa sasa. Tunatafsiri usingizi kinyume na mana halisi…na hivyo tunaamini kufumba macho na kutoamka ni usingizi huku ikiwa siyo kweli.

Kuna baadhi ya vigezo ni lazima vizingatiwe tunapoongelea usingizi wenye afya, Kama ifuatavyo.

Kikawaida uwezo wa kusinzia unatakiwa uwe unaongezeka kadiri siku inavyoisha, yaani kadri jua linavochwea basi uwezo wa kusinzia huwa unaongezeka na kuwa mkubwa zaidi wakati usiku unapoingia, kinyume na hapo dhahiri kwamba utakuwa umekosa usingizi kiafya.

Usumbufu/kelele ni kitu chochote ambacho kinaharibu ama kuingilia usingizi, kiwango cha usumbufu/kelele kikiwa kikubwa kuliko uwezo wa kusinzia basi ni wazi kwamba utapata shida kusinzia.

Usumbufu/kelele zinaweza kuwa kwenye aina tatu, usumbufu/kelele za kimazingira, usumbufu/kelele za kimwili na usumbufu/kelele za `kiakili.

Mchana mwili unakuwa na nguvu na ukiwa na motisha kubwa ili kufanya shughuli zako za kimaendeleo, lakini hali hii inapojitokeza wakati wa usiku basi yatakiwa kutambua kuwa kuna tatizo na linapaswa kutatuliwa.

Aina mojawapo ya usumbufu/kelele ambazo huingilia zaidi usingizi kwa watu wengi ni mfululizo wa fikra mbalimbali yaani msongo wa mawazo ambazo zinakuwa zinazunguka kwenye akili wakati wa usiku na hivo kuingilia upatikanaji wa usingizi mtamu, ni dhahiri kuwa ukiwa una msongo wa mawazo upatikanaji wa usingizi huwa ni wa shida sana kwani akili inakuwa inawaza sana hadi kuathiri uwezo wa kupata usingizi.

Aina nyingine ya usumbufu/kelele za kimwili ni kama  maumivu ya viungo, shida kwenye umen`genyaji wa chakula, madhara ya matumizi makubwa ya vidonge, na mabaki ya caffeine iliyotokana na unywaji wa kahawa nyakati za jioni.

Pia Usumbufu/kelele wa kimazingira kama vile sauti za redio, mtu anayekoroma, milio ya magari na Wanyama, na zingine nyingi zinazotuzunguka kwa kiasi fulani husababisha mtu kukosa usingizi.

 

Video: Mwanamke mwenye misuli zaidi duniani
Athari za kutumia dawa bila kufanya uchunguzi, kupata ushauri kidaktari

Comments

comments