Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza jeshi la polisi kumtafuta Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa ili asaidie kutoa taarifa za kupotea kwa Mdude Nyagali maarufu kama Mdude aliyedaiwa kuchukuliwa kwa nguvu akiwa ofisini kwake na watu wasiojulikana.

Hayo yamezungumzwa Leo Mei 6, 2019 Bungeni Dodoma wakati Masauni akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Msigwa juu ya kutekwa kwa Mdude na juu ya polisi kukataa kufungua jalada la kesi hiyo.

”Mheshimiwa  Msigwa amelithibitishia bunge kuwa mtu huyu ametekwa bila shaka yeye anataarifa hizi kwahiyo  nielekeze polisi wamtafute Mhe. Msigwa ili awasaidie polisi”. Amesema Masauni.

Masauni amesema kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekwenda polisi kutoa taarifa akidai kuwa ameshuhudia namna mtu huyo alivyotekwa na risasi kama ambavyo inadaiwa.

Hivyo ameagiza pia jeshi la polisi kuwakamata watu wa karibu wa Mdude kulisaidia jeshi la polisi kutoa taarifa zake akiamini kuwa wanafahamu nyendo zake.

Aidha, Masauni ameliambia bunge kwamba Mdude kweli haonekani na hajatekwa kama ambavyo inadaiwa.

Ameongezea kwamba milango ipo wazi kwa jeshi la polisi hivyo yeyote mwenye taarifa kamili afike polisi ili kuripoti tukio hilo.

Makamu wa Rais azindua ripoti ya hali ya mazingira nchini
Msilete siasa kwenye shughuli za kitaaluma- Dkt. Ndugulile

Comments

comments