Winga machachari kutoka Klabu ya AS Roma, Mohamed Salah amesaini mkataba mnono wa miaka mitano kwa majogoo wa Anfiled Klabu ya Liverpool akitokea Klabu ya AS Roma ya nchini Italy.

Aidha, mkataba huo umegharimu dau la pauni milioni 39 kiasi ambacho kinamfanya kuwa mchezaji ghali kusajiliwa katika Klabu hiyo ya majogoo hao ambao wamekuwa wakijidhatiti kila msimu.

Salah mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Misri amesema kuwa amefurahishwa sana kusaini mkataba huo kwani alikuwa na ndoto kubwa za kutinga uzi wa majogoo hao wa Anfiled.

“Ninafuraha sana kuwepo hapa, na nitajitoa kwa asilimia mia moja kwaajili ya Klabu hii, kiukweli nitafanya kila niwezavyo ili niweze kushinda kitu nikiwa na Klabu hii,”amesema Salah.

Alichosema Nikki wa Pili kuhusu tamko la Rais Magufuli kwa wanafunzi
Video: Ben Pol amaliza utata picha zilizozua gumzo, aachia video ya 'Tatu'