Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (Kampuni ya Vodacom Tanzania) wameipongeza timu ya Simba SC kutwaa ubingwa wa ligi hiyo msimu huu 2019/2020. Pia kampuni hiyo imezipongeza timu zote zilizoshiriki VPL msimu huu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom, Linda Riwa, amesema soka ni mchezo pendwa na muhimu sana hapa nchini na duniani kote.

“Tunajivunia sana kuwa sehemu ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kwani inaendelea kukua na kuboreshwa mwaka hadi mwaka. Pongezi zetu pia ziwaendee viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi, klabu zote shiriki, waandishi wa habari, wadhamini wenza pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu katika Ligi Kuu mwaka huu,” amesema Riwa.

Amesema hiyo ni katika kuwapa burudani wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla, kutoa nafasi za ajira kwa wachezaji na watendaji pamoja na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa jamii na nchi tofauti.

“Kama mnavyojua mpira wa miguu (Soka) ni fursa kubwa ya ajira kwa vijana na tunafurahi na kujivunia kuwa sehemu ya mafanikio tunayoyaona kutokana na udhamini wetu ambao umewezesha baadhi ya wachezaji kama Mbwana Samatta na Simon Msuva kupata fursa za kucheza nchi za nje na kufika ulaya,” aliongeza Linda ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.

Kocha Mkuu Simba SC Sven Ludwig Vandenbroeck, Katibu Mkuu Dr. Arnold Kashembe , Kocha Msaidizi Selemani Matola na Kocha wa viungo Adel Zrane.
Picha: Simba SC watua Dar es salaam
Ibrahimovic ajimwambafai, ajiita Rais wa Milan