Diamond Platinumz anaendelea kudhihirisha kuwa ndiye msanii mwenye mashabiki wengi zaidi au anayefuatiliwa zaidi Afrika Mashariki, baada ya takwimu rasmi kuonesha kuwa wimbo wake ‘Salome’ ndio unaoongoza kwa kuangaliwa zaidi kupitia YouTube nchini Kenya.

Takwimu rasmi zilizotolewa na BBC zimeonesha kuwa Salome ndio wimbo ulioangaliwa zaidi nchini humo ukifuatiwa na ‘Work’ ya Rihanna akiwa na Drake.

Wimbo huo uliowekwa YouTube Septemba 18 mwaka huu umeshaangaliwa zaidi ya mara milioni 9.85.

Orodha ya nyimbo hizo inaoensha kuwa video za nyimbo za Watanzania zina nafasi kubwa zaidi nchini Kenya huku jicho likielekezwa zaidi kwa wasanii wa kundi la ‘WCB’

Hii ni orodha kamili ya nyimbo zilizoangaliwa zaidi YouTube nchini Kenya:

Salome – Diamond Platnumz na Raymond

Work – Rihanna na Drake

Bado – Diamond Platnumz na Harmonize

Sauti Sol – Unconditionally Bae, na Alikiba.

Work from Home – Ty Dolla Sign na Fifth Harmony

This is What You Came For – Calvin Harris

Kwetu – Raymond

Cheap Thrills – Sia na Sean Paul

Pillow Talk – Zayn

Ain’t Your Mama – Jennifer Lopez

Some tips on crafting a reliable research paper produce educational essays
Beach Soccer: Tanzania Yaitambia Uganda