Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua Kampeni ya utoaji chanjo ya kudhibiti saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike wenye umri kati ya miaka 9 hadi 14.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo ya uzinduzi Makamu wa rais, amesema kuwa ni jambo jema kwa Taifa kuwa na wananchi wenye afya na kuwalinda watoto katika magonjwa hatarishi.

Aidha Makamu wa Rais amewaagiza Waganga Wakuu na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kupima saratani ya matiti na ya mlango wa kizazi.

Amesema kuwa Utoaji wa Chanjo dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi pamoja na uchunguzi wa awali kwa pamoja vitasaidia kuwakinga mabinti na kubaini mapema ugonjwa wa saratani kwa wanawake na hivyo kuepusha maumivu makali ama vifo vinavyoweza kuzuilika.

“Tunatakiwa hadi Desemba, 2018 tuwe tumewafikia wanawake milioni tatu. hii itawezekana endapo kila mmoja wetu ataweka kipaumbele katika kufikia lengo hilo,”amesema Samia Suluhu

Hata hivyo, Makamu wa Rais ameongeza kuwa Serikali itatoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi bila malipo yoyote katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo vya Serikali, Mashirika ya Dini na Taasisi Binafsi

 

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 11, 2018
Nusu fainali ASFC kuchezwa Aprili 20, 21