Sanamu ya mchezaji  wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi limekutwa limevunjwa na watu wasiojulikana likiwa limebakia na sehemu ya chini ya kiuno huku sehemu ya juu ikiwa haipo.

Sanamu hilo lililopo mji wa Buenos Aires, Argentina lilijengwa kwa ajili ya kumshawishi Messi kurejea katika timu ya taifa baada ya kutangaza kustaafu limekutwa likiwa nusu na mhusika wa tukio la kuvunja sanamu akiwa bado hajajulikana.

Hata hivyo watendaji na viongozi wa soka nchini humo wamesema tayari wameanza utaratibu wa kuirejesha kwenye hali yake ya kawaida..

“Sanamu hiyo ya Lionel Messi imekutwa imevunjwa na taarifa za awali zinasema ni uvunjaji wa makusudi ambao hauhusiki na vuguvugu zozote za kisoka au kisiasa,” mamlaka za serikali na jiji za Buenos Aires zilisema kwenye taarifa.

“urekebishaji wake kwa sasa upo kwenye mkakati na umeanza kufanyika.”

Sanamu hiyo ipo katika eneo maarufu la “Paseo de la Gloria” akiwa pamoja na wanamichezo wengine kama mcheza tenisi Gabriela Sabatini na mchezaji wa NBA na bingwa wa Dunia, Manu Ginobili akiwa miongoni mwao wenye sanamu.

Serikali yakamilisha mkakati wa magonjwa yasiyo ambukiza
Ney wa Mitego: Epuka kampani ambazo si rafiki na ndoto zako

Comments

comments