Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Sekta ya Elimu ya Juu imepata mafaniko makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la udahili na uimarishaji mifumo ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

Amesema hayo wakati wa kufunga maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ambapo amesema idadi ya wanafunzi wa Shahada ya kwanza kwenye vyuo vya Elimu ya juu imeongezeka kutoka 65,064 mwaka 2015/16 hadi 87,934 mwaka 2020/21 huku

Naibu Waziri Kipanga amesema katika kuhakikisha Vyuo Vikuu vinatoa elimu bora ya kiushindani ndani na nje ya Nchi, mifumo ya uthibiti ubora imeendelea kuimarishwa ikiwemo mifumo ya ukaguzi na ufuatiliaji na mifumo ya uhakiki na utambuzi wa sifa za kitaaluma za wahitimu wa Elimu ya Juu zilizotolewa na vyuo vya nje ya nchi.

“Pamoja na mafaniko hayo makubwa pia tumeboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu ikiwemo ujenzi na ukarabati wa madarasa, kumbi za mihadhara, maabara, maktaba, hosteli na ununuzi wa vifaa vya utafiti, pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia,” amesema Kipanga

Ametoa wito kwa vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu kuendelea kufanya mapitio ya mitaala ili iendane na mahitaji ya soko la ajira kwa kuweka msisitizo katika masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM), pamoja na utoaji wa mafunzo kwa vitendo.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Charles Kihampa amesema maonesho ya mwaka 2021 yamekuwa na mafanikio makubwa kwa kupata washiriki wengi na kwamba zaidi ya waombaji elfu 52 wa Shahada ya kwanza wametuma maombi katika vyuo mbalimbali na kati ya maombi hayo mengine yamefanyika moja kwa moja kupitia maonesho.

Wapo sokoni, kuwasajili 'RUHSA'
UCSAF yatakiwa kudhibiti manunuzi na usambazaji wa vifaa vya TEHAMA mashuleni