Timu ya taifa ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ kesho  inatarajiwa kuondoka jijini Dar es Salaam, Tanzania kesho Septemba 22, 2016 kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya kambi ya siku 10 kabla ya kuivaa Congo-Brazzaville katika mchezo wa pili kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Baada ya Serengeti Boys kushinda mabao 3-2, jijini Dar es Salaam, timu hizo zinatarajiwa kurudiana Oktoba 2, 2016 huko Congo Brazzaville na timu itafayopata ushindi wa jumla katika michezo miwili itafuzu kwa fainali hizo.

 

Uamuzi wa kuoa ni ujasiri wa watu wachache, wengi wao ni waoga.
Kilimanjaro Queens Kurejea Kesho