Waziri wa michezo wa Italia Vincenzo Spadafora, amethibitisha Ligi Kuu nchini humo (Serie A) itarejea mnamo Juni 20.

Serie A ilisitishwa mnamo Machi 9, huku mabingwa watetezi Juventus FC wakiongoza msimamo wa ligi, wakisaliwa na mizunguuko kumi na mbili kumaliza msimu huu wa 2019/20.

Wachezaji wa klabu shiriki za ligi hiyo, tayari wamesharejea kwenye mzoezi ya pamoja mwezi huu, baada ya kufanya mazoezi binafsi kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu kusimamishwa kwa ligi hiyo, kwa ajili ya kupisha mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.

Mei 20, Shirikisho la soka nchini Italia (FIGC) liliweka wazi tarehe ya mwisho ya kumaliza msimu huu wa 2019-20 kuwa ni Agosti 20.

FIGC pia ilisema ililenga madaraja Matatu ya juu kuhitimisha na kwamba ikiwa ligi yoyote kati ya madaraja hayo haitoanza tena, mfumo wa playoff utachukua nafasi.

Aua mtoto wa siku mbili baada ya kutelekezwa na mwanaume
Zitto kutumikia kifungo cha kutotoa matamshi ya uchochezi mwaka mmoja

Comments

comments