Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa wito kwa aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kutoa taarifa zinazohusu magaidi wa Al – Qaeda kwa Jeshi la Polisi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alipokuwa alipogusia suala la usalama hususan katika kipindi hiki cha mvutano wa marudio ya uchaguzi wa Zanzibar.

“Kuna nchi za jirani ambazo zimekumbwa na madhara ya ugaidi, sasa kama kuna watu kama akina Lowassa na wengine wenye maono kama hayo au kuwa na taarifa za ziada za magaidi basi wapeleke Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi,” alisema.

Hivi karibuni, Lowassa alitahadharisha kuwa kuna uwezekano Zanzibar ikatumiwa kama njia ya kuingia magaidi wa Al – Qaeda endapo jitihada za kutafuta amani visiwani humo zitashindikana na amani kuvunjika.

Waziri Mohamed alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuhakikisha amani iliyopo inaendelea kudumishwa. Alisema Serikali hiyo imejipanga pia kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa agizo za Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhusu kurudia uchaguzi.

Simba, Yanga, Azam FC Zaendelea Kukwepana Kombe La Shirikisho
Utafiti: Farasi hubaini hisia za binadamu kwa kumuangalia