Kumekuwa na kitendawili juu ya uwezo wa wanyama kuweza kutambua hisia za binadamu kwa kuwaangalia, huku ikielezwa kuwa ni mbwa pekee ndiye mnyama ambaye angeweza kutambua hisia kwa mtindo huo.

Lakini hivi karibuni, Wana sayansi wa Chuo Kikuu cha Sussex cha Uingereza wamefanya utafiti na kubaini kuwa farasi wana uwezo pia wa kubaini hisia za binadamu aliyekasirika au mwenye furaha kwa kumuangalia tu.

Wanasayansi hao walitumia picha za wanaume wenye tabasamu na wengine wenye hasira na kuwaonesha farasi 28 waliochaguliwa kufanyiwa majaribio na walitoa majibu sahihi.

Amy Smith ambaye alishiriki katika utafiti huo alieleza kuwa farasi walionesha hali ya uoga walipoona picha ya mwanaume aliyekasirika, na walitulia walipoona picha ya mwanaume aliye tabasamu.

Ilielezwa kuwa farasi walioneshwa picha ya mtu aliyekasirika waliiangalia kwa jicho la kushoto zaidi. Sayansi inaonesha kuwa akili za wanyama zimeumbwa katika hali ambayo hisia zinazotolewa na jicho la kushoto huangaziwa na eneo la kulia la ubongo ambalo hutumiwa kuangazia hisia mbaya.

Kadhalika, watafiti hao walieleza kuwa farasi waliooneshwa picha ya mtu aliyekasirika, mapigo yao ya moyo yalienda mbio zaidi ya pale walipooneshwa picha ya mwanaume aliyetabasamu.

 

 

 

 

Serikali ya Zanzibar yamuomba Lowassa kutoa taarifa kuhusu Al - Qaeda
Mchungaji Msigwa aushangaa uamuzi huu wa Rais Magufuli