Wizara ya Afya imetoa tahadhari juu ya uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikana Mkoani Kagera katika Wilaya ya Bukoba Vijijini ambapo Watu  saba  waliripotiwa kuwa na dalili za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi huku watano kati yao wakifariki na wengine wawili wakiendelea na matibabu.

Taarifa hiyo, imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu katika Ofisi za Wizara zilizopo jijini Dodoma na kuongeza kuwa walipokea taarifa za uwepo wa ugonjwa ambao bado haujajulikani  Kagera,  Bukoba Vijijini, Kata ya Maruku na Kanyangercko, Vijiji vya Bulinda na Butayaibega.

Amesema, mwenendo wa ugonjwa huo una ishara ya uwezekano wa kuambukiza, na kwamba  Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuweza kuchukua hatua za kudhibiti na usisambae na kuwataka Wananchi kuwahi kituo cha kutolea huduma za afya kwa ajili ya uchunguzi na matibabu endapo wataona dalili za kupatwa na homa, kutapika, kuharisha, kutoka damu na mwili kuishiwa nguvu.

Aidha, Prof. Nagu pia amewakumbusha Wananchi kuwahi Kutoa taarifa mapema kwenye kituo cha kutolea huduma za afya kilicho karibu, au kupiga simu namba 199 bila malipo endapo watamuona au kukutana na mtu mwenye dalili kama hizo.

Waziri wa uchukuzi awasilisha barua ya kujiuzulu, Rais akubali
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 17, 2023