Rais wa Zambia, Edgar Lungu ametangaza hali ya dharura nchini humo kutokana na moto mkubwa uliyoteketeza soko kuu nchini humo lililopo mjini Lusaka.

Rais Lungu amesema kumekuwa na visa mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kuteketea kwa soko hilo, ambapo ameeleza kuwa ni vitendo vya kuhujumu uchumi ili kuifanya Zambia isitawalike vyema.

Moto huo unaodhaniwa kuanzishwa kwa makusudi, umeteketeza bidhaa nyingi zilizo kuwa katika soko hilo.

Hata hivyo, wapinzani nchini humo  wamesema kuwa Rais Lungu anatumia mikasa hiyo kama kisingizio cha kuendeleza utawala wa kiimla.

Awali, Wakati tukio hilo likijiri, mashuhuda wameeleza kuwa huenda moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme na kuwalaumu vikosi vya zima moto kwa kuchelewa kufika kuzuia moto huo kusambaa.

Soko hilo lina wafanyabiashara wengi zaidi nchini Zambia. Kati ya bidhaa zinazouuzwa ni pomoja na nguo za mitumba, vifaa vya elektroniki na hata chakula.

JPM afanya uteuzi mwingine
Mwijage azikingia kifua bidhaa za ndani