Mwanaume mmoja mkazi wa Jijini Dar es salaam, Vicent Marseli (37) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kinondoni kwa kukabiliwa na shtaka la kumshika sehemu za siri mtoto wa miaka mitatu ili kujiridhisha hisia zake za mapenzi.

Mwendesha mashtaka wa Jamhuri, Neema Moshi, amedai kuwa mnamo februari 18 eneo la Mbezi Beach mshtakiwa alifanya shambulio hilo la aibu kwa kumshika mtoto sehemu za siri ili aljiridhishe kimapenzi.

Kwa uande wa mshtakiwa amekana kutenda na kuhusika na tendo hilo, jambo lililo pelekea mwendesha mashtaka wa jamhuri kuomba tarehe ya kutajwa tena kesi hiyo kwani upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Kwa upande wa hakimu aliyeendesha keshi hiyo amesema kuwa dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaotoa bondi ya shilingi za kitanzania 50,000 kila mmoja, hata hivyo mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande.

Rais Magufuli afanya uteuzi wa viongozi
Mbivu, Mbichi ya wabunge kujiongezea posho Kenya kujulikana Julai