Mlinda mlango wa klabu ya Stoke City Jack Butland, anatarajia kufanyiwa upasuaji mdogo, kufutia jeraha ya kifundo cha mguu ambalo limekua likimsumbua kwa muda wa miezi sita.

Butland aliumia kifundo cha mguu alipokua katika majukumu ya timu ya taifa ya England, wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa dunia timu ya taifa ya Ujerumni, ambayo ilikubali kufungwa mabao matatu kwa mawili.

Upasuaji huo utafanyika mwanzoni mwa juma lijalo (Jumatatu), na utamuweka nje ya uwanja mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa muda wa miezi miwili.

Image result for Jack Butland injuredJack Butland

Hatua hiyo itaendelea kumpa ulaji mlinda mlango mpya wa klabu ya Stoke City Shay Given, wa kukaa langoni katika michezo ya msimu huu wa 2016/17.

Hata hivyo ilitarajiwa huenda Butland angekua fit kabla ya kuanza kwa msimu huu, lakini mambo yaliendelea kuwa tofauti na ndipo kitengo cha utabibu cha Stoke City kiliposhauri afanyiwe upasuaji mdogo.

Mamadou Sakho Amalizana Na Klopp, Asajiliwa Kikosi cha PL
Video: Majaliwa katika mkutano wa 6 TICAD - Makala