Ikiwa waislamu wote duniani wanaendelea mfungo wa kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan na leo ikiwa ni chungu cha 28, Mufti na  Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Bin Zuber Ally Mbwana amesema kuwa sikukuu za Eid El-Fitri zitasherekewa siku ya Ijumaa June 15, 2018 au Jumamosi Juni 16, 2018.

Amesema siku hizo mwezi unatarajiwa kuandama kama ilivyo desturi ya sikukuu hii ambayo huadhimishwa mara baada ya mwezi kuandama ambapo ametangaza kuwa ibada ya sikukuu hii itaswaliwa ndani ya viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Aidha kuelekea kusherekea siku hii maeneo ya masoko yakiwemo Kariakoo yamefurika na watu mbalimbali kwa ajili ya kufanya manunuzi ya chakula na mavazi kwa ajili ya kusherekea Eid El-Fitri.

Baraza linawatakia sikukuu njema ya Eid El-Fitri na kuwatakia amani tele katika kusherekea siku hiyo.

 

 

Tuzo ya mchezaji bora VPL 2017/18 kutua Msimbazi
Nchemba afafanua kuhusu haki ya mtuhumiwa