Mchezaji wa Simba, Sharaf Shiboub ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Sudan.

Shiboub amejumishwa katika kikosi hicho ambacho kitacheza michezo miwili ya kufuzu AFCON 2021 dhidi ya Sao Tome  Novemba 13  na Novemba 17 watacheza na Afrika Kusini.

Wakati Shiboub akisafiri kuelekea Sudan kwa ajili ya kibarua hicho, hapa Tanzania, Kocha Mkuu wa Taifa Stars ametangaza kikosi kwa ajili ya mechi za kufuzu AFCON pia dhidi ya Libya na Guinea.

Katika orodha hiyo, jumla ya wachezaji saba wa Simba wameitwa katika kikosi hicho ambao ni Mohamed Hussein, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Miraji Athumani na Hassan Dilunga.

Wakati huohuo  mshambuliaji mwingine wa Simba wa Meddie Kagere amesema kuwa hakuna raha yoyote anayoipata kufunga mabao yake kwani anakamiwa na wapinzani mwanzo mwisho akiwa ndani ya uwanja.

Kagere ni kinara wa ufungaji wa mabao ndani ya ligi kuu bara akiwa amefunga jumla ya mabao nane mpaka sasa kwenye michezo nane ambayo Simba imecheza.

“Hakuna raha kwenye kufunga kwani ninapitia magumu mengi ikiwa ni safu ya mabeki ambao kwa sasa wananitazama kwa ukaribu, nafurahi kuona namna ninavyofunga kwaajili ya timu hivyo siangalii idadi ya mabao bali naangalia ushindi tunaopata.

“Suala la kufunga mabao sio langu peke yangu ni kwa kila mchezaji ndio maaana tunacheza tukiwa timu, kitu kikubwa kwetu ni ushindi,” amesema Kagere.

Wizi wa kura 2015 wamfikisha Msigwa kamati ya maadili
Waziri asisitiza elimu matumizi ya gesi