Wadada wengi  huvaa sana na kujali sana muonekano wa juu zaidi kuliko kuangalia nini anachotaka kuvaa chini kama kinaendana na kile anachovaa juu ili kuwa na muonekano mzuri.

Wataalamu wanashauri kuwa kwa mwanamke mwenye mguu mnene ni bora kuvaa kiatu ambacho hakina kifundo ili kisigawe mguu wake juu na chini na kuleta picha mbaya ya mguu, ambapo unashauriwa  kuvaa kiatu chenye ncha mbele na uwazi ili kuleta muonekano mzuri zaidi.

Lakini pia kwa uchaguzi wa viatu angalia rangi ambayo haitakuwa inan’gaa sana katika miguu yako, jaribu sana kuvaa rangi zinazoendana na ngozi ya mwili wako na si vinginevyo.

kwa wanawake wenye miguu mirefu ni vizuri kuvaa kiatu che kifundo inapendeza zaidi, lakini pia kiatu kirefu cha kamba kinakuwa na muonekano mzuri kwa watu wa aina hii.

kwa wenye miguu miembamba, unashauriwa sana kuvaa kiatu chenye wedges ili kufanya miguu yako kujaa  na kuonekana imependeza katika kiatu husika.

kwa  wenye miguu mifupi,  vaa kiatu kirefu cha kuchongoka mbele na pia kiwe na uwazi kwa nyuma au mikanda.

Fanya haya uonekane mrembo siku zote
Video: Kinana, Makamba sasa shubiri CCM, Diwani CCM alivyonaswa na rushwa

Comments

comments