Vinara wa msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara timu ya Simba Queens, kesho Jumatano itashuka dimbani ikiwa mwenyeji wa Mlandizi Queens kwenye Uwanja wao wa Mo Simba Arena, Bunju jijini Dar es Salaam.

Simba Queens ambayo ipo kileleni ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 17 wakati huu wakiwa wamebakiza mechi tano kabla ya kuhitimisha msimu, mwishoni mwa juma lililopita iliacha kipigo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya Kigoma Sisters, katika mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Katika mchezo huo ambao Malkia hao wa Msimbazi waliutawala kwa sehemu kubwa, walipata mabao yote matatu kipindi cha kwanza yakifungwa na Mwanahamisi Omari dakika ya 10 na Oppa Clement aliyetupia mawili dakika ya 16 na 40.

Bao pekee la kufutia machozi la Kigoma Sisters liliwekwa kimiani na Kadosho Shaban kwa mkwaju wa penati dakika ya 89.

Michezo mingine ya Ligi Kuu ya Wanawake mzunguuko wa 18 itakayochezwa kesho Julai 22/2020

Tanzanite vs Baobab, Alliance vs TSC, Marsh vs Kigoma, Ruvuma vs Panama na JKT vs Yanga

Mtibwa Sugar Vs Young Africans "Pasua Kichwa"
Fahamu yaliyopewa nafasi kwenye magazeti leo, Julai 21, 2020