Uongozi wa Klabu ya Simba unaujulisha umma kuwa aliyekuwa Kocha wa makipa Muharami Said Mohammed maarufu ‘Shilton’ , hakuwa muajiriwa wa klabu hiyo na wala hakuwa na mkataba na Simba.

Simba ilimuomba Muharami kuwanoa makipa wake kwa muda kwa mwezi mmoja, wakati huo klabu ikiendelea kutafuta Kocha wa kudumu.

Kwa mantiki hiyo klabu haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo na klabu iko tayari kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika pindi itakapohitajika kwa maslahi ya Taifa.

Uongozi wa Simba unawaomba mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yeyote kwa klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo.

Wakati huo huo Simba SC imemtangaza Zakaria Chlouha raia wa Morocco Kuwa Kocha Mpya wa Walinda Lango.

Kabla ya kutua Simba, Zakaria Chlouha mwenye umri wa miaka 48 alikuwa akiifundisha Klabu ya Al Urooba kutoka Falme za Kiarabu (U.A.E).

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 16, 2022 
Wataalamu wa Mifugo kujengewa uwezo huduma Vijijini