Katika muendelezo wa kufuta sherehe na maadhimisho mbali mbali ya Serikali ambayo huwa yanafanyika kitaifa, yanazidi kushika ambapo leo kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene kutangaza kuahirishwa kwa Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani.

Maonyesho hayo yalitarajiwa kufanyika kitaifa jijini Dar es salaam,Desemba 3, mwaka huu yameahirishwa na badala yake kila mkoa utaadhimisha kivyake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene amesema maadhimisho hayo yalilenga kila halmashauri isafirishe wanachama wa vyama vya watu wenye ulemavu ili washiriki maadhimisho hayo jijini humo.

Aidha, Simbachawene amesema kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa wakuu wa mikoa kuwa badala ya maadhimisho hayo ya kitaifa kukusanya walemavu wote kwenye mikoa kwenda Dar es salaam yafanyike kwenye mikoa yao

Waziri Mkuu aongoza viongozi na wananchi kuaga mwili wa mzee Pinda
Mbadala Wa Dani Alves Aanza Kusakwa