Siri ya kikao cha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu  na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Edward Lowassa kilichofanyika jijini Dar es salaam kilikuwa kwaajili ya Nyalandu kumshukuru mjumbe huyo.

Baada ya kukutana na kufanya mazungumzo, Nyalandu amesema kuwa lengo kubwa la kukutana na mjumbe huyo lilikuwa ni kwaajili ya kumshukuru kwa kuonyesha njia kwa wengine kuwa kuna maisha nje ya CCM.

Aidha, Nyalandu alijiondoa ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa madai kuwa chama hicho kimepoteza mwelekeo, hivyo kukihama na kuomba kujiunga na Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA.

“Mzee wangu nimekuja kusema asante kwa kutufungulia mlango wa kuweza kuangalia maisha mengine nje ya CCM, kwani naamini mwaka 2020 tutavuka na kutimiza malengo,”amesema Nyalandu

 

Hata hivyo, kwa upande wake, Edward Lowassa amesema kuwa amefarijika sana kwa hatua zilizochukuliwa na mbunge huyo wa zamani wa Singida Kaskazini ya kukihama chama alichokuwa akikitumikia, hivyo amesema kwa ushirikiano wa pamoja wataweza kuleta mabadiliko.

Trump atoa onyo kali kwa Rais wa Korea Kaskazini
Video: Siri ya kikao cha Nyalandu na Lowassa Dar, Deni la Taifa lapanda