Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amemtembelea aliyekuwa Mgombea urais wa UKAWA 2015, Edward Lowassa ofisini kwake, Mikocheni Jijini Dar es salaam na kupanga namna ya kuimarisha umoja ndani ya upinzani.

Nyalandu ametumia mtandao wake wa kijamii kuweka ujumbe huo akiambatanisha na picha ya kiongozi huyo ambaye kwa sasa ni mjumbe ndani ya kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

“Nimefanya mazungumzo na Mh. Edward Lowassa kuhusu umuhimu wa kuimarisha umoja miongoni kwa vyama vya upinzani nchini. Tanzania kuelekea 2020. Wazee watawalao vyema, wanastahili  heshima  maradufu. Asante sana Mh. Edward Lowassa,”ameandika Nyalandu

Aidha, Nyalandu pamoja na Edward Lowassa wote waliwahi kuwa viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wote tayari wametoka ndani ya chama hicho.

Hata hivyo, Lowassa kwa sasa tayari ni mwanachama wa CHADEMA na Nyalandu tayari ameshaweka nia ya kuhamia CHADEMA tangu alipojiuzulu mapema wiki iliyopita ingawa mpaka sasa bado hajachukua kadi ya chama hicho

Neymar kuwa mrithi wa Ronaldo?
Azam FC yavunja mkataba na Yahaya Mohammed