Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds Fm, Diva amewatolea povu mashabiki waliohoji kuhusu mahojiano yake na mchekeshaji Mama Ashura ambaye alitumia muda mwingi kuukosoa mwenendo wa Alikiba katika muziki wake, wakati inasemekana kuwa Diva ni shabiki mkubwa wa timu Kiba.

Diva amesema yeye hana timu na anaheshimu kazi yake na watu wanapaswa kuelewa kuwa kwa sasa yupo bize sana kutengeneza maisha yake ya baadae hivyo hawezi kushughulika na mambo kama hayo, Diva amesema,

“Nimepata malalamiko baadhi ya watu Oh kwanini umemualika Mama Ashura, wewe si team Kiba Oh Diva this and that”.

”Naomba ni make it very clear mimi sina U team, mambo ya Uteam yanagawa mashabiki wangu, sitaki kwanza hata kusikia mambo hayo tena, Im over that Path. Mungu mwenyewe anajua nilivyo bize saa hii building my life and my future jaman , have alot in my plate sahan yangu imejaa sana”.

Diva amesema huo muda tena hana na yeye ni shabiki wa kila mtu hata wale wanaomchukia yeye anawapenda kwani nao humfanya azidi kuwa maarufu.

“Yes ila sichagui sibagui ataenizika simjui wanasema waswahili, Mi nahudumia watu wote sihudumii pande moja tu, Sitaki Gawa shabiki zangu sababu ya vitu ambavyo havinipi faida maishani, tuendeleeni kuwa marafiki tuheshimiane,”.

Aidha ameeleza kuwa yupo huru kumualika mtu yeyote kwenye kipindi chake cha Ala za Roho kwa namna atavyojisikia yeye na kwa jinsi watu watakavyomuhitaji, amesisitiza kutokuwa upande wowote na ameomba watu waheshimu kazi yake.

Amemaliza kwa kusema,  ”I choose to be happy and means i’ll support good music regardless, na ukinikosea I m free shot you with Nothing but the truth, I m free soul, peace out!!,” amesisitiza.

Hayo ameyaandika kupitia mtandao wake wa instagram.

Video: Barrick watua Ikulu, mjadala wa makinikia waanza rasmi Dar
Mkurugenzi Tume ya Uchaguzi aliyepotea apatikana akiwa amefariki