Mkutano wa 13 wa Bunge umeanza leo Novemba 6, 2018 jijini Dodoma huku wabunge wanne wakiapishwa na Spika Job Ndugai, ambao wote ni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Thimotheo Mzava (Korogwe Vijijini), Mwita Waitara (Ukonga), Julius Kalanga (Monduli) na Zuberi Kuchauka (Liwale).

Wabunge Mwita Waitara, Julius Kalanga na Zuberi Kuchauka, wamekula viapo hivyo baada ya kujivua nyadhifa zao za awali wakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuomba kujiunga na CCM ambapo serikali ililazimika kufanya chaguzi za marudio ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wabunge hao katika majimbo yao ambapo waliibuka washindi kwa mara nyingine tena.

Aidha, Spika wa Bunge, amesema kuwa miswada ya sheria mitano itasomwa kwa mara ya kwanza ikiwemo wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018, mswada mingine ni wa maji na usafi wa mazingira, marekebisho ya sheria mbalimbali namba nne wa mwaka 2018, muswada wa mamlaka ya hali ya hewa wa mwaka 2018 na wa mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu.

Katika mkutano huo wa 13, mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa mwaka 2019/20 utajadiliwa na sehemu kubwa mijadala itajikita katika mpango huo lakini pia maswali 125 yataulizwa na ya papo kwa Waziri Mkuu yatakuwa 16

Kidole cha mke wake champeleka jela maisha
Stuart Baxter atii amri ya Thulani Serero

Comments

comments