Timu ya Stand United chini ya udhamini wa kampuni ya Acacia imedhamiria kufuata nyayo za Azam katika soka la Tanzania.

Timu hiyo ya Shinyanga imeamua kujikita rasmi katika uibuaji, ukuzaji na uendelezaji wa chipukizi kama moja ya mkakati wao wa kuwa moja ya timu bora nchini na barani Afrika.

Mkurugenzi wa benchi la ufundi wa timu ya soka ya Stand united ya mkoani Shinyanga Mujibu Kanu amesema kuwa timu yake ina mikakati mikubwa katika kuinua soka la vijana mkoani hapo pamoja na nchi nzima kiujumla.
Akizungumza na Soka 360 Kanu alisema lengo lao kwa sasa ni kushirikiana na mdhamini wao wa Acacia katika kuhakikisha wanainua soka la Vijana.

Kama timu chini ya udhamini wetu wa acacia tumeamua kuhakikisha timu inaendelea kufanya vizuri katika ligi kuu Tanzania bara na kubaki ndani ya tano bora,kama ilivyo kusudio la Acacia kuinua Stand united ili iweze kuja kuwa timu bora nchini na Africa.Ili hayo yatimie lazima pia tuwekeze kwenye Soka la vijana

 

Mradi huo una madhumuni ya Kujenga kikosi imara cha vijana ili kuepuka upotevu wa pesa nyingi ambazo hutumika katika kununua wachezaji toka timu tofauti kuja Acacia Stand United.

Tutaanza na mpango wa kuzunguka nchi nzima kutafuta chipukizi ambao siku zijazo wataisaidia Acacia Stand united kufikia malengo na kuwatafutia soko nje na mwisho wa siku Soka la nchi yetu litakua kwa kuongeza nyota wanaocheza katika ligi zenye ushindani mkubwa na tutaitangaza Acacia stand United na vijana watakua wamepata ajira

Chanzo: soka360

 

Angalia Orodha Ya Klabu 10 Bora Barani Afrika
Azam FC Nje Ya Azam Complex Mwezi Mmoja