Kikosi cha Liverpool kesho kitashuka dimbani kucheza mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Hoffenheim bila ya washambuliaji Daniel Sturridge na Philippe Coutinho.

Sturridge alikosa mchezo wa kwanza wa ligi ya nchini England mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Watford, kufuatia majeraha ya paja aliyoyapata wakati wa kujiandaa na msimu mpya.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ameachwa katika safari ya kuelekea nchini Ujerumani iliyosheheni wachezaji 22 wakiongozwa na meneja Jurgen Klopp.

Kuachwa kwa kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil Coutinho, kumeendelea kuibua hisia tofauti kuhusu mustakabali wake huko Anfield, hasa baada ya kuibua sokomoko la kutaka auzwe kwa kuwasilisha maombi maalum mwishoni mwa juma lililopita.

Coutinho anawaniwa na FC Barcelona kwa lengo la kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mbazili mwenzake Neymar aliyetimkia nchini Ufaransa kwa matajiri wa jijini Paris PSG, majuma mawili yaliyopita.

Ronaldo afungiwa michezo mitano Uhispania
Video: MCT Yatangaza ripoti ya uvamizi Clouds Media