Baada ya ukimya wa zaidi miaka mitano mfululizo, akiwa nje ya sanaa ya muziki, hatimaye mwanamuziki nguli wa Hip hop nchini, Joseph Mbilinyi maarufu ‘Sugu’ amewataarifu mashabiki na wapenzi wa kazi zake juu ya ujio wake mpya ifikapo Februari 14, 2022.

Kupitia ukurasa wake maalumu wa mtandao wa Instagram ambapo Sugu ameandika,

“Too much PRESSURE, wengine wanasema itoke fasta hata audio, wengine wanasema tusubiri video, naomba mnivumilie kidogo tufanye mambo mazuri, maana mmesubiri ngoma mpya kwa miaka 6 sasa, so ni vema tuwe na a proper comeback… Sasa expected WORLD PREMIER ni FEB. 14 🙏🏾🙏🏾 #TAITA.”


Sugu anatangaza rasmi ujio huo, ikiwa ni zaidi ya miaka mitano tangu alipotoa wimbo wake wa mwisho ‘Freedom’  aliouachia tarehe 25 Aprili 2016.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 24, 2022
Rais Mwinyi asisitiza maboresho ya sheria kujenga uchumi wa buluu