Mshambuliaji wa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa Super Mario Balotelli amemkaribisha beki wa Liverpool Mamadou Sakho kwa kumwambia milango ipo wazi kujiunganae.

Sakho amekua hana maelewano mazuri na meneja wa Liverpool  Jurgen Klopp, na huenda akauzwa wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari mwaka 2017.

Balotelli amezungumza na televisheni ya TFI ya nchini Ufaransa na kueleza kuwa, anapendezwa na uchezaji wa Sakho na angependa ajiunge na Nice, endapo atauzwa mwezi Januari.

“Nimekua na mawasiliano na Sakho mara kwa mara, na mara zote amenieleza uwezeoano wa kuondoka Liverpool mwezi Januari,”

“Nimemwambia hana budi kufanya hivyo kutokana na hitaji lake la kucheza kila juma na ninaamini Nice ni mahala tulivu kwake.

“Nimecheza na Sakho, ni mchezaji mzuri na mwenye viwango ambavyo vinahitajika hapa, ningeshauri asajiliwe ili asaidie mipango iliyowekwa kwa msimu huu. Alisema Balotelli.

Balotelli aliondoka Anfield mwanzoni mwa msimu huu na kujiunga na Nice ya Ufaransa, baada ya meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kuweka bayana kutokua na mpango wa kumtumia.

Lukaku: Paul Pogba Anastahili Ballon d'Or 2016
Mauricio Pochettino: Alli Hatokua Nasi Kwa Siku Kadhaa