Kipindi cha runinga cha Take One cha Clouds TV kitarudi hewani mwezi huu baada ya hukumu yake ya kufungiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyotolewa Octoba mwaka 2016 kumalizika mwezi huu.

Kipindi hicho kilifungiwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money  na kurusha kipindi kilichohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

Mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema ametangaza ujio wa kipindi hicho huku akiwataka mashabiki wa kipindi hicho kutoa maoni juu ya mabadiliko ya kipindi hicho.

“Tukiwa tumemaliza likizo yetu tuliyopewa na TCRA, kipindi chetu kinarudi rasmi January hii 2017 namaanisha Take One mtangazaji wako nikiwa yuleyule Zamaradi H. Mketema,” aliandika Instagram Zamaradi.

“Hebu niambie katika msimu wetu mpya unatamani kuona nini kwenye kipindi!!? Unatamani irudi vipi ili kuboreshwa!!? Nini kiongezwe!? Nini kipunguzwe!? Nipe maoni yako tafadhali nami nitayafanyia kazi,”

Kipindi hiko kilirushwa hewani Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00 mchana.

Avram Grant Atangaza Kikosi Cha Ghana
Wafuasi wa chadema kortini Karatu