Tanzania na Brazil zimeingia makubaliano ya kuinua kilimo cha Pamba ili kiwe na tija kwa wakulima nchini.

Makubaliano hayo yamejili wakati ambapo Brazil ipo katika hatua kubwa za kimageuzi ya kilimo huku ikiwa na mafanikio makubwa katika sekta hiyo ambapo unatekelezwa katika nchi tatu za Burundi, Kenya na Tanzania.

Mradi wa kuinua kilimo cha Pamba unaotekelezwa na Brazil nchini Tanzania utajikita Zaidi hasa katika kuhakikisha wakulima nchini wanapata Pamba mbegu bora na uzinduzi wa utafiti utamfikia mkulima ili aweze kuongeza tija.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa ameyasema hayo jana tarehe 11 Machi 2019 mara baada ya kutembelea na kukagua mashamba ya mfano wa kilimo cha Pamba katika kituo cha Utafiti TARI-Ukiriguru Mkoani Mwanza.

Mhe Bashungwa amesisitiza kuwa serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa kauli moja kuimarisha sekta ya kilimo huku katika zao la Pamba imejipanga kuhakikisha inazalisha mbegu vipara za Pamba zitakazotosheleza kwa wakulima wote nchini na kuondokana na utumiaji wa pamba manyoya ambayo imezoeleka lakini tija yake ni ndogo katika uzalishaji kuliko Pamba Manyonya.

Alisema Wizara ya kilimo itakuwa na jukumu la kushawishi wawezaji ili kuwekeza kwenye viwanda vya Pamba nyuzi pamoja na viwanda vya nguo na kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza vyema maelekezo yaliyoainishwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi yam waka 2015-2020.

Aidha, alisema kuwa Serikali pia imejipanga kupanua maabara za utafiti wa zao la Pamba ili kuimarisha ufanisi na tija ya zao hilo kwani mafanikio ya kilimo yanategemea zaidi katika utafiti.

Mhe Bashungwa ameishukuru serikali ya Brazil kwa utekelezaji wa mradi huo nchini Tanzania ambao unatokana na mahusiano mazuri katika nchi hizo mbili inayoakisi katika kufungamanisha kilimo na uchumi wa viwanda.

Kadhalika alisema serikali tayari imeanzisha vituo viwili vya kuzalisha Pamba mbegu vipara katika mkoa wa Simiyu pamoja na Mkoa wa Tabora

Video: Waziri Mpina ateketeza tani 11 za Samaki wenye sumu walioingizwa nchini kutoka China, atoa msimamo mzito
Kisiwa cha Lamu chapiga marufuku matumizi ya Magari, Punda pekee kutumika

Comments

comments