Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo Juni 30, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa kundi la maseneta wa Ufaransa Ronan Dantec.

Moja ya ajenda waliojadiliana katika mazungumzo hayo ni pamoja na umuhimu wa kuhifadhi mazingira lengo likiwa ni  kupunguza hewa mkaa duniani.

Makamu wa Rais, amesema amefurahishwa na namna uhifadhi wa mazingira unavyofanyika nchini ufaransa ikiwemo Mji wa  Paris licha ya ukongwe wa mji huo, amemuhakikishia Seneta Dantec kwamba Tanzania ipo tayari kushirikiana na Ufaransa katika uhifadhi wa mazingira na kuwakaribisha.

Naye, Seneta Dantec ameshauri uwepo wa mfuko wa fidia kwa wale watakaothirika na masuala ya kuhifadhi na kulinda mazingira ambayo itakuwa ni faida kwa upande wa mazingira.

Dkt. Mpango, yuko Nchini Ufaransa kuhudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa (Generation Equality Forum) lililoanza leo Juni 30 hadi Julai 2 ,2021 lenye lengo la kuchagiza haki za usawa wa kijinsia kama zilivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing wa mwaka 1995.

Hayati Mfugale kuzikwa Julai 5
Mchakato wa katiba unachelewesha maendeleo?