Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Paul Rupia (86), ambaye alikuwa madarakani kuanzia mwaka 1986-1995 amefariki dunia hii leo Septemba 16, 2022 nchini Afrika Kusini na taarifa za kifo chake zimetolewa na Mtoto wake Peter Rupia ambaye amesema baba yake alifariki hii leo majira ya asubuhi.

Wakati wa uhai wake, Balozi Rupia amewahi kuwa ofisa katika Wizara ya Mambo ya Nje (1963), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Umoja wa Mataifa na pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Watu.

Balozi Paul Rupia.

Hayati Balozi Rupia alizaliwa Januari 21, 1938 mkoani Shinyanga na ni mtoto wa mpigania uhuru, mfanyabiashara na mwanasiasa wa zamani, John Rupia ambaye alikuwa ni muasisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA) na Tanganyika African National Union ( TANU).

Hata hivyo, taratibu za maziko ikiwemo kurudisha mwili nchini bado hazijatolewa rasmi ambapo huenda wanafamilia wakatangaza hatua zinazofuata baada ya kukaa kikao ili kuutangazia umma maamuzi ya mwisho kabla ya kumpumzisha Kiongozi huyo mstaafu katika nyumba yake ya milele.

Waliofariki kwa mafuriko, shoti ya umeme wafikia 134
Bungeni: Wenye malimbikizo ya madeni 'walegezewa kamba'