Shirika la utangazaji Tanzania ‘TBC’ limetangaza kuanzisha utaratibu wa kuanza kutoa tuzo kwa wasanii wakongwe na kizazi kipya kwa lengo la kutambua thamani na mchango wa wasanii hao katika jamii kupitia kupitia sanaa zao.

Taarifa hiyo imewekwa wazi na mkurugenzi wa shirika hilo, Dkt Ayoub Rioba, alipokuwa katika kipindi cha jambo Tanzania wakati akitolea ufafanuzi kuhusu Tamasha la ‘Tukutane Kwetu’ litakalofanyika Mei 21, 2022.

“Niwashukuru sana wasanii wa Tanzania, ni watu ambao wamefanya kazi muhimu na kubwa sana katika nyakati mbali mbali, na sisi kama Tbc tulikwishaanza kukutana nao tangu mwaka 2020, na tulishakubaliana kuwa tutakuwa tunakutana kila mwaka rasmi,”alisema Rioba.

Aidha ameongea kuwa “Tunapanga kufanya kazi na wasanii wa Tanzania katika namna ambayo huenda haijawahi kuonekana, Kwa hiyo sisi tunapanga kuwa na utaratibu wa kutoa tuzo kila mwaka kuenzi wale ambao kwa muda mrefu walifanya kazi nzuri ili wasisahaulike na jamii,”

“Tumeanza kupiga nyimbo za wasanii miaka ya nyuma kabisa, hivyo lazima tuwapongeze kwa kazi wanazofanya na hii si kwa wakongwe tu hata hawa wapya, lengo ni kutambua mchango wao katika sanaa.” amesema Dkt. Ayoub Rioba.

Mkataba wa Songas kupitiwa upya
FAO kujikita na uboreshaji wa Uvuvi